Maswali Yanayoulizwa Sana kuhusu Ballot Scout

  • Ballot Scout ni programu ambayo inafuatilia kura za ndani zilizotumwa kupitia barua kwa kutumia huduma ya Baakodi za Barua za Posta ya Marekani (USPS), pamoja na data kutoka kwa wasimamizi wa uchaguzi. Ballot Scout iliundwa na Democracy Works, shirika lisilo la faida, na washirika na ofisi za uchaguzi wa mitaa.

  • Tafadhali andika jina lako la kwanza, jina la mwisho, na anwani uliyoomba kura yako itumwe, na ubonyeze Fuatilia Kura Yako (Track Your Ballot). Jina na anwani utakayoandika lazima vifanane na yale maelezo uliyotumia ukijisajili kama mpiga kura.

    Ikiwa inapatikana katika eneo lako la kisheria, unaweza pia kujisajili ili upate arifa.Ili kujisajili, tafuta kura yako, kisha uweke anwani yako ya barua pepe na/au nambari ya simu katika sehemu ya arifa. Unaweza pia kuzima arifa na kuwasha katika sehemu hii wakati wowote. Maelezo yako ya mawasiliano yatahifadhiwa salama na hayatatumiwa kamwe kwa madhumuni mengine yoyote isipokuwa arifa zinazohusiana na hali ya nyenzo zako za kura.

  • Baada ya kujasajili, Ballot Scout itatuma sms na/au barua pepe kura yako inapobadilika hadi hali mpya. Unapojisajili, kura yako tayari imeanza kusafiri, hutapokea arifa za hali yoyote ya awali.

  • Ili kukoma kupokea arifa za sms jibu komesha wakati wowote kwa ujumbe wowote.

    Ili kukoma kupokea arifa za barua pepe, bofya kiungo mwishoni mwa ujumbe wako wowote wa barua pepe unaosoma, “Ili kujiondoa bofya hapa”.

    Ili kusimamisha au kubadilisha jinsi unavyopokea ujumbe, nenda kwenye kifaa, tafuta kura yako, na uwashe au uzime kila aina ya arifa. Unapaswa kupokea uthibitisho wa mabadiliko yako.

  • Jina unaloandika lazima lilingane kabisa na jina ulilotumia ulipojisajili kupiga kura. Ikiwa jina lako limeandikwa vibaya kwenye usajili wako wa mpiga kura, litaandikwa vibaya katika Ballot Scout. Kwa mfano, ikiwa ulijisajili kama “Rob” na si “Robert”, unahitaji kutumia lakabu/kifupisho cha jina lako ili kutafuta kura yako. Vilevile, anwani uliyoweka lazima ilingane na anwani ya barua kama inavyoonekana katika usajili wako wa mpiga kura/kwenye bahasha yako ya kura. Ikiwa una uhakika kuwa umeandika jina na anwani yako sahihi lakini unaendelea kupokea kasoro, tafadhali wasiliana na ofisi yako ya uchaguzi ya karibu ili kuangalia hali ya kura yako.

  • Kwa sasa, hakuna njia rahisi ya ufikiaji ya kufuatilia barua kupitia posta ya jeshi kwa kutumia misimbo ya msingi ya USPS domestic Intelligent Mail. Tunaweza kufuatilia kupitia USPS, lakini pindi tu kura inapoingia kwenye mfumo wa posta wa jeshi, hatuwezi kuiona. Tunaweza kuwapa wasimamizi wa uchaguzi wanaofaa data kidogo ya kufuatilia wakiiomba lakini tumekosea upande wa kutowapa wapiga kura kwa sababu ni data ambayo haijakamilika. Kuna miradi kote nchini inayotafuta njia za kuchangia hili lifanye kazi vizuri na wakati mbinu faafu ya ufuatiliaji iliyojumuishwa imeundwa, bila shaka tutaona jinsi tunavyoweza kuitekeleza!

  • Tafadhali tazama fafanuzi zilizo hapa chini kwa hali zote za kura zinazowezekana. Fahamu kwamba si lazima kila kura ipitie kila hali moja na kwamba vipengele vingine vya hali* (Imetumwa kwenye ofisi, Inasafiri hadi ofisini, Imepokelewa, Imekubalika, Haijakubalika) vinapatikana tu katika maeneo fulani.

    • Inaandaliwa - Kura yako bado haijaingia kwenye barua lakini inaandaliwa na ofisi ya uchaguzi ya eneo lako. Hali hii inawekwa na ofisi za uchaguzi; haihusiani kamwe na data za USPS.

    • Imetumwa kwako - USPS ina kura yako na inaelekea kwenye anwani yako

    • Imeratibiwa Kuletwa - Kura yako iko katika ofisi ya posta ya eneo lako na ina tarehe ya kuletwa iliyokadiriwa. Inapaswa kufika kwenye anwani yako mnamo/takribani tarehe hiyo na barua yako ya kawaida.

    • Imerejeshwa kwa Mtumaji - USPS haikuweza kupeleka kura yako kwa anwani yako. Kura mpya inaweza kuhitaji kutolewa.

    • Imetumwa kwenye Ofisi* - Kura yako iliyokamilika inarejeshwa katika ofisi kupitia posta

    • Imepokelewa na Ofisi* - Kura yako imepokelewa na ofisi ya uchaguzi. Hii inaweza kumaanisha USPS imefikisha kura yako, au kura ilifikishwa kwa mkono au kutumbukizwa sandukuni, kama zinapatikana. Kwa baadhi ya maeneo, hii itakuwa hali ya mwisho ya kura yako.

    • Imepokelewa na Ofisi - Imekubaliwa* - Kura yako imetiwa alama ya kukubaliwa kuhesabiwa na ofisi ya uchaguzi. Hali hii huwekwa na ofisi ya uchaguzi; haihusiani kamwe na data USPS.

    • Imepokelewa na Ofisi - Imekataliwa* - Kura yako inaweza kuwa na tatizo na unapaswa kuwasiliana na ofisi yako ya uchaguzi. Hali hii huwekwa ofisi za uchaguzi; haihusiani kamwe na data USPS.

  • Pindi inapotumwa, kura yako itachukua kati ya siku 2-5 kuwasilishwa. Tafadhali fahamu kuwa, tarehe ya uwasilishaji inayokadiriwa inaamuliwa kulingana na aina ya data ya uchanganuzi ya USPS inayopokelewa wakati kura imetiwa lebo kuwa inawasilishwa kutoka kwenye kituo chako cha karibu cha posta, si kwamba imewasili katika kisanduku chako cha barua.

  • Huenda ukawa katika eneo ambalo Ballot Scout inafuatilia tu kura yako kutoka kwenye ofisi yako ya uchaguzi hadi kwako kwa sababu ofisi ya uchaguzi haikuweza kujumuisha msimbo wa Intelligent mail kwenye kura yako ya kurudi. Hii haimaanishi kuwa kura yako haipo njiani kurudi kwenye ofisi, bali ni kuwa hatufuatilii mchakato huo.

  • Hii haimaanishi kuwa kura yako haisafiri, inamaanisha kuwa haijachanganuliwa tena na USPS. Mara nyingi huenda vituo vinig vya posta visiwe na vifaa vya uchanganuzi ili kuendelea kuchanganua kura au USPS inaweza kupanga kura kwa njia ambayo haihamishi kura kupitia mashine husika za kuchanganua. Ikiwa huna uhakika iwapo unapaswa kuwa umepokea kura yako kufikia tarehe iliyosemwa au ikiwa ofisi inapaswa kuwa imepokea kura yako, tunakuhimiza uwasiliane na ofisi yako ya uchaguzi ya karibu au ya jimbo.

  • Kwanza, hakikisha kuwa barua zako zote za siku zimewasili. Kura zitawasili pamoja na kuwasili kwa barua yako kwa kawaida, si katika uwasili tofauti kama uwasili wa kifurushi cha faragha. Kisha, hakikisha kuwa kura haijawasili katika bechi ya barua kutoka siku nyingine. Wakati mwingine bahasha za kura zinaweza kudhaniwa ni barua taka! Ikiwa barua yako ya siku imewasili na hujaipata bahasha, wasiliana na ofisi yako ya uchaguzi wa karibu kwa nambari uliyopewa. Huenda ikawa USPS iliwasilisha kura yako kwenye anwani isiyofaa au haikuwasilishwa na huenda ukahitajika kupewa kura mpya.

  • Kwa sababu za usalama, tunatumia toleo kuu la sasa la kila kivinjari na toleo moja la awali. Ikiwa unakumbana na matatizo kutumia Ballot Scout, jaribu kusasisha kivinjari chako hadi toleo la sasa.

  • Tunatunza vizuri ili kuhakikisha kuwa taarifa za mpiga kura zinasalia kuwa za siri. Hatuuzi taarifa za mtumiaji wala kusambaza data binafsi yoyote kwa madhumuni yoyote ambayo si kukupa taarifa na huduma ambazo umeomba. Kwa maelezo zaidi kuhusu sera yetu ya usalama, tafadhali tembelea ukurasa wetu wa sera ya faragha na masharti ya huduma.

JE, UNA MASWALI MENGINE? TUPO HAPA KUSAIDIA.